Nisaidie, nina huzuni na upweke

Na sijui jinsi ya kuwa bora

Una huzuni na upweke? Hauko peke yako. Ni kawaida kuhisi hivyo. Labda una huzuni kwa sababu ya jambo linalotendeka maishani mwako, kama kufeli mtihani au kumtamani mtu unayempenda. Au labda unafadhaika kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wako. Hapa kuna mambo unayoweza kufanya uhisi bora...

Mtazamo mzuri: Ni vigumu kuwa na mtazamo mzuri wakati unahisi umetengwa na kila kitu karibu nawe inahofisha. Lakini inakubidi ujaribu kujikumbusha mambo yote yanayokufanya uwe wa ajabu. Mambo kama kuwa mkarimu, kutoogopa kuanza upya unapokosea jambo au jambo jingine ambalo wewe ni bora.

Kuwa na shajar piahusaidia. Andika mambo yanayokufanya bora, kama nukuu za kutia motisha kuhusu thamani yako, nguvu na madhumuni. Fanya jambo ndogo kila siku na utakuwa bora katika muda usiokuwa mrefu. Ukikwama kuhusu jambo la kuandika kujihusu, zungumza na wazazi au mlezi wako na umuulize sifa zako nzuri.

Pata hobby: Jiunge na klabu au anza moja. Kukaa na watu kama wewe ni bora kwa furaha na kuijiamini kwako. Tuseme unapenda kusoma; anza klabu ya kusoma na kuchambua vitabu inayokutana kwenye maktaba yenu mtaani au shuleni. Unaweza pia kujaribu vikundi vya michezo na sanaa.

Tenda mema: Tazama jamii yako. Kuna shirika linalohitaji watu wa kujitolea? Au jaribu mtaa wako. Kuna mkongwe anayehitaji mtu wa kumsaidia kwenda sokoni au mtu anayehitaji usaidizi na kazi za nyumbani. Kabla ya kutenda mema, kumbuka kwamba usalama wako unatangulia. Pata mtu mzima unayeamini, kama mzazi au mwalimu, kukusaidia kupata shirika bora au mtu wa kusaidia.

Iondoe moyoni: Mwambie mtu mzima unayemwamini kinachoendelea ndani yako. Uwazi wa hisia zako ni mbinu bora ya kuanza kupona. Kama huna mtu mzima unayemwamini maishani mwako, pigia simu msaidizi wa watoto mtaani au tembelea hospitali.

Ukiwa na msaada unaofaa, mambo yatakuwa mazuri.

Share your feedback