Kumbatia upungufu wako!
Unahisi kama kwamba hufai? Hivyo ni vizuri! Ulizaliwa ili kuwa wa kipekee! Siku hizi watu wana wasiwasi sana kuhusu kufaa hivi kwamba wanasahau kinachowafanya kuwa wa kipekee. Kwa nini uwe kama kila mtu ilhali unaweza kuwa wewe!
Ng`aa kama almasi, msichana!
Inuka wengine wanapoanguka.
Usipoteze wakati kuhofia kuhusu kile ambacho watu wengine wanafikiria kukuhusu au kuhisi kukosa usalama kwamba hufai. Pro-tip: Ni mawazo yako tu. Hakuna kiwango, kila mtu anafaa. Kila mmoja anakabiliana na — na kuangazia — hisia zake sawa za kukosa usalama. Kwa hivyo jitahidi na utulie kwa sababu u bora kwa kuwa ulivyo, hakuna mwingine anayeweza kulifanya bora zaidi.
Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba.
Mojawapo ya vitu bora zaidi kuhusu kuwa mtu binafsi ni kwamba tunaishia kufahamu watu wengine waungwana wanaofanya mambo yao binafsi. Nyote mnaelewa kuhusu kukumbatia upungufu wako na sifa bora. Ni vyema kuwa na marafiki wengine wa nje kwa sababu sio tu kwamba una mtu anayejua mapambano, bali pia una marafiki ambao ni bora kwa kufanya mambo mbalimbali. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu dunia na mambo mbalimbali yanayovutia, jambo linalotupeleka kwenye hoja yetu inayofuata.
Tofauti ni za ajabu!
Watu wengine huchora. Watu wengine hucheza densi. Watu wengine huimba. Watu wengine huringa. Unaelewa. Na wewe? Fanya chochote kinachokufurahisha mradi tu usimkwaze mtu mwingine. Wewe si duni wala mwenye thamani zaidi kuliko marika yako kwa sababu kila msichana ni wa kipekee kabisa na tofauti na mwenzake. Ni kama kulinganisha matofaa na nyati. Zama kwenye upungufu wako, boresha vipaji vyako binafsi na utafurahi zaidi.
Fikiria ikiwa dunia ingejaa watu wanaofanya vyema mambo sawa kwa vivutio na nguvu na udhaifu sawa. Inaudhi, sivyo?
Share your feedback