Wewe hufanya nini mabadiliko yanapoonekana kuwa mageni

Mazoea mapya na mfuatano? Tunaweza kufanya hivyo!

Watu huchukia neno "mazoea", lakini kwa kusema ukweli kabisa, wa kuaminika? Mazoea yanawezakuwa ya ajabu. Kwa mazoea mimi huwaona rafiki zangu shuleni, ambapo tuna mazoea ya kutembea na kuzungumza na kupanga mipango ya wikendi. Mazoea yangu ni pale ambapo mimi hufanya mambo yote ambayo hakika huyafanya maisha yangu kuwa ya ajabu sana wakati mwingine.

Iwapo mazoea hayo yatabadilishwa...kusema ukweli, huwa ninakasirika sana.

Hivyo nini hufanyika mazoea yanapobadilika? Na sio kidogo tu, lakini sana? Shule zinaweza kufungwa, au huenda nikakosa kuwaona rafiki zangu. Labda mtu wa familia kuwa mgonjwa, au labda niko katika mahali papya kabisa?

Ukweli ni kuwa, huwa ninaelewa mabadiliko haya ya mazoea ya kawaida kuwa magumu kabisa. Haya hapa ni baadhi ya mambo ambayo mimi hujaribu kufanya ili kuyafanya mambo kuwa rahisi kidogo.

Kukubali kuwa mambo yanabadilika

Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe! Iwapo yale ambayo ulikuwa umezoea kuyafanya kila wiki ghafla ni tofauti, hatuwezi kuendelea na kujifanya kama hakuna kilichotokea. Hivyo, vipi ukichukua muda kukubali kuwa maisha yamebadilika na inavyomaanisha kwako.

Ni sawa kuhisi

Hata unapokubali mambo, ni sawa kabisa kuhisi kukasirika kuhusiana nayo. Mambo mengi hatuwezi kuyazuia. Kukubali huchukua muda, hivyo jipe muda wa kupumzika ili kuchanganua unavyohisi. Niamini, hii kwa kweli husaidia!

Izungumzie

Baada ya kuelewa kuwa hisia zetu zinafaa, tunaweza kuzungumza kuhusu jambo hili na wazazi wetu, marafiki wetu, au hata katika shajara zetu. Kushiriki kunaweza kusaidia kumaliza wasiwasi wetu.

Tafuta vipaumbele

Kwa watu wengi, kuzishughulisha akili zetu kwa mambo ya kufanya hukuruhusu kushughulikia mabadiliko makubwa kwa urahisi zaidi. Iwe kazi ya shuleni, mambo uyapendayo, au hata mazoezi ya mwili: jaribu kupata mambo yanayokufanya kutabasamu katika siku yako, Kumbuka, hii ni tofauti kwa kila mmoja, hivyo usijali iwapo yako ni tofauti na ya rafiki.

Mazoea ya “Kitambo” na mapya

Sawa, hivyo huenda kuna baadhi ya mazoea ambayo ni wazi kuwa hutaki tu kuyaachilia. Hiyo ni kawaida kabisa. Badilisha ya zamani kwa mapya! Unakosa kuzungumza na rafiki zako shuleni? Weka tarehe ya simu ya video au SMS alasiri.

Tafuta mazuri

Maisha sio kitu kingine isipokuwa mabadiliko. Umri wetu huzidi kuongezeka, mambo tunayoyapenda huwa mengi, ujuzi wetu huwa bora zaidi na ulimwengu wetu kuwa mkubwa zaidi. Mabadiliko sio burudani kila wakati, lakini kila wakati ni fursa ya kuhisi jambo jipya.

Mabadiliko yanaweza kuwa magumu. Jipende na ujikubali, na ufanye tu yale ambayo unaweza kuyafanya.

Share your feedback