Nilifikiri alikuwa rafiki mbaya

Lakini nilikuwa nimekosea!

Tumekuwa marafiki na rafiki yangu wa dhati Ana tangu siku ya kwanza shuleni. Nilikuwa na woga kwa hiyo daima alinishika mkono na kunisaidia kuwa jasiri.

Karibia mwisho wa mwaka uliopita, Ana alianza kuwa tofauti. Kila wakati nilipotaka kujifurahisha – alikuwa anakataa. Alianza kukataa kila kitu nilichosema. Hata alianza kunishinikiza nisiende kujiburudisha na marafiki zangu.

Nilifikiria labda alikuwa na wivu. Nilipata mpenzi na nilikuwa nimeanza kutengeneza urafiki na marafiki zake.

Ilikuwa inakaribia likizo na mpenzi wangu na marafiki kadhaa walikuwa wanapanga kwenda kununua chakula kwenye soko la usiku na kwenda kujiburudisha. Nilimualika Ana lakini alikataa – tena.

Tulianza kubishana. Nilimwambia nilikuwa nimechoka kujaribu kumualika kila wakati na anakataa. Nilikuwa tayari kukata tamaa.

Ana alianza kukasirika. Nilimwambia aniambie tatizo liko wapi na akaanza kuniambia kwa nini hakuwa anafurahia kuwa na kundi lile.

Ana alisema kwamba alikuwa amesikia uvumi kwamba kundi lile walikuwa wanakunywa pombe walipoenda kujiburudisha. Hakutaka kujihusisha nalo wala hakutaka pia mimi nijihusishe nalo.

Sikuwa na fahamu kwamba kulikuwa na uvumi na nikamwambia Ana kwamba sikuwa nimeyaona mambo yale. Nilimuahidi kwamba ikiwa lile lingetokea ningemshika mkono na tuondoke pamoja papo hapo! Jinsi alivyonifanyia tulivyokuwa watoto.

Sasa ninajua kuwa wazi na Ana na ninapoona mabadiliko katika tabia zake ninamwambia haraka iwezekanavyo – bila kukubali iendelee kwa wiki kadhaa.

Ana siyo rafiki mbaya, alitaka tu sote tusipatwe na matatizo. Ninafurahi sana tulizungumza na tuna uhusiano wa karibu kuliko awali!

Share your feedback