Kuweka akiba kunaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako

Hadithi ya Nandi

Nandi alikuwa na ndoto ya kutengeneza mifuko ya kitambaa ya kupendeza ya kuweka kalamu ambayo angeweza kuwauzia marafiki na wanafamilia wake. Alikuwa mbunifu kila mara na ana kipawa cha mitindo na alitaka kugeuza uchu wake kuwa biashara ya kutengeneza pesa. Alikuwa na ujuzi wake wa kushona, lakini alihitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kununua vifaa.

Ilimlazimu Nandi kujifunza jinsi ya kuweka bajeti na kuweka akiba pesa alizokuwa akipata kutokana na kazi ya kutunza watoto na kusaidia katika kuuza kwenye duka lililokuwa katika eneo lake. Ilikuwa vigumu, lakini ilileta mafanikio na kwa sasa mifuko yake ya kuweka kalamu ni maarufu zaidi!

Nandi alitumia Mpando wa Kuweka Akiba wa Hatua 4 ili kufanikiwa:

1. Chagua lengo la kuweka akiba
Nandi alibainisha kiasi kamili cha pesa ambazo alihitaji ili kuanza biashara yake. Alijua kuwa alitaka kuanza kwa kutengeneza mifuko 20 ya kuweka kalamu ili kujaribu mpango wake wa kwanza wa biashara. Aliorodhesha gharama ya nyenzo ambazo angehitaji na zipu au vifuasi vyovyote. Pia aliongeza gharama ya vifaa vya kushona kama vile sindano na uzi. Hatua ya kuongeza vitu hivi vyote pamoja ilimpa kiasi cha jumla ambacho kilikuwa lengo lake la kuweka akiba.

2. Kutengeneza mpango wa kuweka akiba
Ili kutengeneza mpango wa kuweka akiba, ilimbidi Nandi kufanya hesabu ya gharama zake za kila mwezi. Aliongeza pamoja mapato aliyotarajia kupata kutokana na kazi yake ya kutunza watoto na kazi za dukani. Kisha aliondoa kiasi cha pesa ambazo mamake angetaka kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Alifikiria kuhusu vitu vya maana ambavyo angehitaji na pia kuondoa gharama ya vitu hivi. Kiasi kilichosalia ndicho ambacho angehifadhi kila mwezi.

3. Jua tofauti kati ya mahitaji na vitu vya ziada
Ili kuhakikisha kuwa amefuata mpango wake wa kuweka akiba, ilimbidi Nandi kuwa na uhakika kuhusu mahitaji na vitu vya ziada. Nguo mpya haikuhitajika, lakini marashi na dawa ya mswaki vilihitajika. Nandi aligundua kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo ni vya umuhimu na vingemsaidia katika afya na masomo yake. Hivi ndivyo vitu alivyohitaji na alijua kuwa alihitaji kuvipa kipaumbele kuliko vitu vingine vya ziada kama vile vitafunio au vifuasi vya nywele.

4. Dhibiti matumizi
Nandi alifikiria kuhusu njia zingine ambazo angetumia kudhibti matumizi yake ili aweze kufuata mpango wake wa kuweka akiba na kufikia lengo lake la kuweka akiba. Alipangia mapema shughuli ambazo angeweza kufanya na shughuli ambazo zingemgharimu zaidi. Alianza kuwa mbunifu na kupanga mambo ambayo angeyafanya na marafiki zake katika muda wake wa ziada kama vile kupanga klabu ya mjadala shuleni.

Hatua ya kujifunza jinsi ya kuweka akiba ya pesa zako ili kutimiza ndoto inaweza kuwa ngumu lakini yenye manufaa!

Share your feedback