Sanaa ya kuachia huru

Wakati mwingine hakuna fursa ya pili — na hilo ni sawa.

Mwaka mpya umefika!

Ni wakati wa watu wengi kutafakari. Pia ni wakati wa mianzo mipya. Kila mwaka, tunajiambia njia zote kuwa tutabadilika: mwaka huu nitakuwa mvumilivu zaidi, nitakuwa mkarimu zaidi, nitasoma kwa bidii, nita...

Subiri! Acha! Usituelewe vibaya: ni muhimu kuwa ‘wewe’ unavyoweza, ili kuweka mipango na malengo. Lakini pia ni muhimu kutafakari jinsi tunavyowatendea wengine, na mwaka mpya ni wakati bora wa kufanya hilo.

Wakati wa hadithi!

Anya na Busi wenye miaka kuni na saba walikuwa marafiki wa dhati. Walienda pamoja kama chanda na pete. Kila kitu kilikuwa sawa, hadi wazazi wa Busi walipomhamishia shule tofauti.

Kwanza, Anya na Busi waliweza kudumisha urafiki wao kupitia simu za kila mara, kuwasiliana kwenye WhatsApp siku nzima, na kila mmoja kulala kwa mwingine wikendi.

Hatimaye, hata hivyo, Busi alianza kupata marafiki wapya kwenye shule yake mpya na alikuwa na muda kidogo wa kukaa na Anya. Simu zilikaa kutoka kila siku hadi kila wiki hadi kukosa kupigwa kabisa. Busi alishughulika na marafiki zake wapya na Anya akakwazika. Nafasi yake ilikuwa imechukuliwa?

“Nilihisi kana kwamba sikuwa mtu kwake,” Anya alisema kwa mshangao, “Ilionekana ni kama Busi alinisahau pindi tu alipopata marafiki wapya.” Alimpeza Busi. Alipeza kuwa na mtu aliyemwelewa — na akakasirika kwa sababu Busi hakuonekana kujali kamwe.

Ungalikuwa Anya, ungalimsamehe Busi na kusonga mbele?

Ni kama huna budi kufanya hivyo. Mambo hutendeka. Watu hubadilika. Watu hutengana. Wakati mwingine watu hutukwaza bila hata kutambua hilo. Sehemu ya kukua inamaanisha kutambua kwamba hatuwezi kudhibiti jinsi watu wengine wanavyotenda mambo; tunaweza tu kudhibiti hisia zetu kwa watu wengine.

Ni sawa kuhuzunika mtu anapokukwaza. Kutengana na rafiki wa dhati ni jambo baya — kulia ni kawaida na hata kwenye afya zaidi. Lakini pia ni muhimu kuachia huru machungu na mambo mabaya, baada ya kutoa hisia zetu. Lazima tuendelee na maisha, na hatutaki hasira kutuzuia kusonga mbele.

Hivyo, Anya alifanya nini? Alimwendea Busi na kumwambia alivyohisi. Unajua kilichotoke? Busi alishangaa sana! Hakukusudia kumkwaza Anya, na alimpeza pia.

Urafiki wa Busi na Anya ulibadilika na hata ingawa mambo hayakuwa sawa tena bado walipendana. Busi alifurahi kuwa Anya alimwamini zaidi kumwambia kuhusu suala hilo na Anya alitambua kwamba moyo wa ukweli na wa kusamehe unaweza kufanya mambo ya ajabu sana.

Share your feedback