Fanya mazungumzo kuendelea
Je! Umewahi kuanza mazungumzo ambayo yaliisha baada ya dakika 5 kwa sababu haukua na kitu kingine cha kusema? Ndio! Sote tumepitia hapo. Hasa inapofikia wakati wa kuzungumza na watu wakubwa kama wazazi, walinzi au washauri.
Unapowaza kuhusu hili, hakuna haja ya kuaibika au kuwa na wasiwasi kuhusu hali isiyo ya kawaida. Unahitaji tu kuwa mbunifu katika maswali yako. Kwa mfano, kukosa kujua cha kumuliza mshauri sio sababu ya kukosa kutafuta mshauri. Hofu ya kuzungumza na watu ni hisia ambayo kila mtu anapitia, lakini hio haitakufanya uwe mwanamke aliyefanikiwa ambaye unataka kuwa siku za baadaye.
Washauri ni watu wenye ujuzi ambao husaidia kuongoza watu wenye ujuzi mdogo katika mambo muhimu maishani. Mara nyingi wanakuhimiza kufungua macho na mawazo yako na kuona mambo kwa mtazamo tofauti. Wanaweza kuleta utofauti mkubwa sana maishani mwako ikiwa utazingatia ushauri wao katika hali za kila siku. Wanasema "mafanikio huwa na ishara" na mazungumzo na washauri yanalenga kusababisha haya! Hivyo uliza maswali yanayofaa. Sikiliza vidokezo na ishara wanazotoa. Watumie katika maisha yako na kukua, kukua, kukua! Haitakaa kuwa wazo mbaya, sivyo?
Ikiwa unang’ang’ana kufanya mazungumzo na mshauri wako, hapa kuna maswali mazuri ambayo yataleta msisimko na kuendeleza mazungumzo!
Uliwezaje kupata kazi yako ya sasa?
Ulijifunza vipi jinsi ya kukabiliana na kushindwa?
Je! Kulikuwa na nafasi ya kazi ambayo uliomba na ukapata, lakini haukuwa umefuzu 100%?
Je, ni nini huwa unazingatia unapofanya maamuzi?
Kwa mtazamo wako, ni wapi nina uwezo, na nafaa kuzingatia nini ili kujiboresha?
Ni ujuzi mpya upi ninaohitaji ili kuendelea mbele?
Share your feedback