Jinsi ya kutumia vizuri mawaidha ya mshauri wako

Fahamu jinsi unavyoweza kuwa bora zaidi.

Mshauri ni mtu anayeshiriki ufahamu na uzoefu wake nawe, unayeshauriwa.

Yeye hufanya hivi kwa sababu lengo lake ni kukusaidia utimize malengo yako na ufanikiwe. Kwa hivyo, ni kwa manufaa yako kuchukulia mawaidha ya mshauri wako kwa makini.

Lakini wakati mwingine hutajua jinsi ya kutumia ushauri wake.

Ili kukusaidia tumeweka njia hizi 3 muhimu za kuanza kutumia unachoambiwa na mshauri wako.

1.Wajibika

Mshauri mzuri atakupatia kazi za kufanya. Kazi hizi zinaweza kuwa kitu chochote kuanzia kuandika mpango wa biashara hadi kusoma kwa saa 3 kila siku.

Ili kunufaika kutoka kwa kazi kama hizo itabidi uwajibike kwa kuhakikisha kwamba unatia bidii uwezavyo.

Kwa kufanya hivyo kunaweza kukusaidia kujifunza mengi kuhusu biashara yako au kukusaidia kukuza utu wako.

2.Kuwa tayari kujifunza na kufanya makosa

Utaweza kupata matokeo bora tu kutoka kwa mshauri wako ikiwa uko tayari kujifunza kwa sababu ukweli ni kwamba mshauri wako ana ushauri mzuri unaoweza kuufuata. Amekuwa hapo na akaweza kufanikiwa.

Mshauri wako hatakutarajia uwe kamili. Watu wengi waliofanikiwa wanajua kwamba watafanya makosa mengi katika njia yao ya ufanisi.

Kwa hivyo kuwa na ujasiri wakati unajifunza na kuwajibika badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu kufanya makosa. Ukikosea, usijilaumu sana, kumbuka ulichoshindwa kufanya na ukitumie kama njia ya kujifunza na kuinuka ili uwe bora wakati mwingine.

3. Anza kutumia ushauri wake Haraka Uwezavyo

Kuchelewa na kupoteza muda huchelewesha ufanisi; punde tu mshauri wako anapokupa kazi, tupilia mbali uoga na wasiwasi, jiamini na uruhusu vipawa vyako vya ajabu kukuongoza katika njia ya ufanisi.

Ikiwa unataka kufanikiwa ni muhimu ulenge hisia zako nzuri badala ya hisia zako mbaya.

Hisia zako nzuri hujumuisha hisia za furaha, msisimko, imani, shukrani, mvuto na msukumo. Ukimchagua mshauri sahihi anapaswa kukusaidia katika kuboresha hisia zako!

Mshauri mzuri atajivunia na kufurahia kufanya kazi na wewe ili kukusaidia kuwa bora uwezavyo. Kuna kitu unachokitaka, sio?

Mshauri anaweza kuleta mengi katika maisha yako, punde tu ukimpata anayefaa utaona utofauti. Sasa nenda nje na umtafute mshauri wako anayefaa!

Share your feedback