Kukua, Si Kutengana

Urafiki unaweza kuwa wa karibu — na kuwa mbali zaidi — bila kutengana

Mabadiliko ni sehemu kamili ya maisha ya kila siku. Hutokea kila siku kwa kila mtu. Tunabadilika wakati huu! Mabadiliko ni kila kitu, ni sehemu ya kawaida ya kuwa binadamu.

Lakini je, urafiki wenu ukibadilika?

Inaweza kutendeka kwa ghafla unapokua, na inaweza kuudhi kabisa! Siku moja wewe na marafiki zako mko pamoja kwa saa 24 na siku 7, siku inayofuata, thibitisho! kila mtu ameenda zake akifanya jambo jipya na la kusisimua bila wewe. Umi amejiunga na bendi, Tri anaangazia kufanya kazi na timu yake ya kandanda, na Dewi anajihusisha zaidi kusaidia kwenye kanisa lake.

Inaonekana kila mtu anaendelea na maisha na kutoshughulika na urafiki kabisa - kila mtu isipokuwa wewe. Na hilo linakufanya uone wivu na kuhuzunika, jambo ambalo kwa kweli, ni Sawa kabisa. Ni kile unachofanyia hisia hizo ambacho ni muhimu.

Urafiki ni bora kwa sababu ni kama raba, unaweza kunyumbuka mbali bila kukatika. Huenda ukahisi kama kwamba umewapoteza kabisa, lakini hilo ni jambo zuri kuhusu urafiki, unaweza kuimarika tena. Hakuna kitu kinachokwisha kabisa!

Badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya urafiki wenu, jaribu kutafuta mambo yanayokuvutia. Tafakari wewe ni nani! Ni dunia kubwa, na ndio mwanzo wa mambo. Utashangazwa na watu wote utakaokutana nao njiani, na hali mpya utakazopitia.

Kisha uingie na marafiki zako! Fahamu wanachokifanya. Shiriki kuhusu mambo yote ambayo umekuwa ukifanya, na uwaulize wanachokifanya. Utafahamu kuwa watu uliowajali bado ni wale wale, wamekuwa tu wakijitambua — na urafiki wenu utaimarika hata zaidi.

Unaona? Ulikuwa na wasiwasi tu bila sababu!

Share your feedback