Kabiliana na wadhalimu

Jinsi ya Kukabiliana na Dhuluma ya Mtandaoni.

Intaneti ni eneo bora zaidi. Unaweza kujieleza. Unaweza kushiriki hadithi, mawazo, na hisia, na kuungana na marafiki popote duniani!

Marafiki wa Dhati Milele Duniani? Ndiyo!

Lakini kuna mambo unayopaswa kufahamu. Kwanza kabisa, Intaneti ni eneo la umma. Mambo unayoshiriki hapo yanaweza kutazamwa na marafiki, familia na hata watu wengine usiowajua kabisa. Usipichunga, huenda ukavutia makini hasi kutoka kwa watu katili na hata wadhalimu wa mtandaoni. Kwa hivyo unapaswa kufanya nini ukijipata katika hali kama hii?

Tulia
Usiwe na wasiwasi. Usijibu. Kwa kweli, mambo yatakuwa Sawa. Pumua tu. Sasa pumua tena. Ukipokea maoni ya chuki au ya kutisha, yapuuze. Ripoti akaunti hiyo, kisha uwazuie.

Kama tu katika maisha halisi, wadhalimu wanatiwa moyo wanapokuona ukikasirika. Na pia kama tu katika maisha halisi, puuza wenye chuki. Usiwape sababu yoyote ya kuondoa furaha kwa kutumia Intaneti. Kweli? Wadhalimu wengi wa mtandaoni wanapata njia ya kuteka makini.

Prrrrt! Ikomeshe!
Ikiwa unamjua mtu anayekudhulumu na unamwona kila siku shuleni, mwambie akome. Lakini akiendelea kukudhulumu, wasiliana na mtu mzima mara moja kwa usaidizi kama vile mwalimu au mshauri. Mdhalimu anaweza kutumwa na kufukuzwa shuleni, kutegemea kile ambacho amekifanya.

Hali Inazidi Kuwa Mbaya
Ikiwa unafikiri kuwa umefanya kila kitu na bado unadhulumiwa, kwanza kabisa, unapaswa kuwaambia wazazi wako au mtu unayemwamini kile kinachotendeka. Pili, kuwa jasusi bora na uhifadhi ushahidi wote wa tarakilishi endapo utahitajika kuripoti dhuluma kwa mwalimu wako au hata polisi.

Dhuluma ya mtandaoni ni hatari sana kwa wasichana na wanawake, hivyo sote tufanye juhudi ya kumlinda kila mmoja dhidi ya wadhalimu wa mtandaoni na tuwe wakarimu kwa kila mmoja mtandaoni.

Huendelea kuwa bora
Kudhulumiwa mtandaoni kunaweza kukufanya kuhuzunika, lakini usijali.

Fikiria kwamba si wewe peke yako. Kuna watu wengi sana wanaokujali: walimu, wazazi, na marafiki zako wa dhati! Unaweza kuwakimbilia ukijipata kuwa mwathiriwa wa dhuluma ya mtandaoni. Na pia fikiria kwamba kuna mamilioni ya wasichana wengine ambao wamepitia mambo ambayo umepitia. Na kwa sababu ni kama wewe, wanakupigania ili uyashinde.

Unaweza kufaulu, msichana!

Share your feedback