Jinsi ya kuwa hodari katika jambo hilo ambalo umelitaka daima kijifunza!
Je, una kitu ambacho umetaka daima kujifunza lakini hujawahi kupata nafasi? Pengine ni kupamba keki, kucheza gita, kucheza densi katika onyesho, kupaka picha rangi au kukuza mboga zako mwenyewe.
Tatizo ni, hujawahi kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo. Sasa ni wakati mzuri wa kujiamini na huruhusu talanta yako kung'aa. Ikiwa kwa mara ya kwanza hutafanikiwa, jaribu, jaribu, jaribu tena. Tunapenda msemo huu kwa sababu huzungumzia kuhusu kutokufa moyo!
Jaribu vidokezo hivi na uanze leo:
Mtafute mtu unayemjua au kumpenda ambaye ana kipawa cha kile unachotaka kujifunza. Mwulize kama angependa kukupatia mashauri au akuruhusu umwafilie kwa siku chache ili upate maelezo ya thamani ya mambo anayofanya. Usiogope kuuliza maswali mengi, hata kama unafikiria ni maswali ya kipumbavu.
Tafuta mafunzo mtandaoni au tafuta kozi katika eneo lako ambalo unaweza kuhudhuria. Utashangazwa mambo mengi unayoweza kujifunza kutoka kwa mafunzo ya mtandaoni na mara nyingi huwa bila malipo! Ikiwa inawezekana kwako, kuhudhuria kozi kunaweza kufungua milango mingine pia, unaweza kukutana na watu wazuri sana na pengine kupata nafasi ya kuwa mkufunzi au kupata ajira.
Kumbuka kwamba mtu unayempenda hakuzaliwa akiwa mzuri katika kipawa chake, alijitahidi kwa bidii ili kujifunza ustadi wake na kufika mahali alipo leo. Huenda kuna wakati katika maisha yake ambapo hakuwa na motisha au wakati kila mtu alikuwa mzuri kumshinda, sisi wote tuna siku hizo. Jambo muhimu la mafanikio ni kuendelea hata wakati kuna changamoto na nyakati ngumu na usife moyo.
Elezea familia au mhudumu wako kuhusu ujuzi unaotaka kujifunza, kwa nini unaupenda na utakachofanya ili kujifunza mengi. Njia nzuri ya kuunda uhusiano nao ni kuwaomba msaada wakati unauhitaji, au waeleze utashukuru kwa mchango wowote amba unaweza kuutoa.
Kwa hivyo, kwa kuwa sasa umeamua utakuwa hodari katika ndoto zako, kumbuka kwamba sisi wote tuna siku nzuri na siku mbaya. Lenga uzuri, sahau ubaya na uonyeshe kila mtu jinsi una kipaji!
Share your feedback