Tunza sehemu zako za siri

Kuhusu Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa na Zaidi

Mawazo yako (1)

Unajua jambo? Ujauzito siyo madhara tu ya kufanya mapenzi bila kinga. Unashangaa?

Hebu tuseme umefanya mapenzi bila kinga na kwa bahati nzuri hukupata ujauzito usiotaka. Hili halimaanishi kuwa wewe ni “salama” moja kwa moja. Kuna kile tunachoita maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STI) yanayoweza kuleta madhara. Hata mengine ni madhara ya muda mrefu kama vile vidonda vya ngozi, kupooza, kupofuka, na tatizo la kiungo.

Kuna hata baadhi ya Magonjwa ya Zinaa yasiyoonyesha dalili moja kwa moja, kama vile klamidia, kisonono, kaswende, malengelenge na hata VVU. Ikiwa hujui kuwa umeambukizwa, unaweza hata kuusambaza kwa wapenzi wako.

Maambukizi haya yanaweza kusababisha maumivu makali katika sehemu ya ukeni, utasa/ugumba, na hata kifo.

Hivyo ikiwa tayari unafanya mapenzi, hakikisha kuwa umejikinga ili kupunguza uwezekano wa kupata Magonjwa ya Zinaa.

Suala jingine muhimu zaidi katika afya ya ngono ni kuwa wazi kwa mpenzi wako kuhusu historia ya kufanya mapenzi ya kila mmoja. Usiaibike; ni kitu ambacho kitawafaidi nyote wawili. Pimweni pamoja na daktari ili kujua ikiwa yeyote kati yenu ana Ugonjwa wa Zinaa, na hivyo hamtakuwa mkisambaziana maambukizi ya aina yoyote. Mbali na hili, pia unaweza kuamua kutumia uzazi wa mpango, ambao unaweza kupata kutoka kwenye kliniki au kituo cha afya ili kuepuka kupata na kusambaza Magonjwa ya Zinaa, njia bora ikiwa ni mipira.

Ikiwa unadhani kuna uwezekano mkubwa kwamba huenda una Ugonjwa wa Zinaa, usiwe na wasiwasi. Nenda kwenye kliniki au hospitali ili upimwe. Mtafute daktari wa kuaminika ambaye unaridhika naye. Kuwa mkweli kwake ili ufanyiwe vipimo na kupewa dawa inayofaa. Ukiwa na huduma sahihi ya matibabu, mambo yanaweza kukuwia mazuri.

Share your feedback

Mawazo yako

Njoki

Kutka uchafu mweupe kila siku inamaana uko mgonjwa?

Machi 2, 2024, 3:20 p.m