Usiamini kila kitu unachosikia.
Kuanza hedhi yako wakati mwingine kunaweza kuhisi kwa kutisha. Kuongeza kwa mfadhaiko huu ni hadithi za zamani kuwa hedhi ni chafu. Hii si kweli, lakini inaweza kutufanya tujihisi wapweke. Ukweli ni kwamba, hedhi hutokea kwa nusu ya idadi ya watu duniani, na sio chafu au kitu cha kuonea aibu! Kukumbuka mambo haya machache kunaweza kukufanya jasiri Zaidi kuhu hedhi, na kupunguza wasiwasi wowote wa hedhi.
1. Hedhi ni sehemu ya afya njema ya maisha!
Hedhi ni kawaida kabisa na sio chafu kwa njia yoyote. Kwa kweli, kupata hedhi yako ni ishara ya afya njema. Ni kazi ya kiasili ya mwili na kitu ambacho watu duniani kote wanapitia. Ndio, hata mwanamuziki wako mashuhuri wa kike, bingwa wa filamu, mwalimu, au mwanasiasa. Kuzungumza na marafiki wako kuhusu hedhi yako ni njia nzuri ya kujisikia jasiri na kupunguza upweke. Unaweza hata kuwasiliana na mwanamke mzee aliyeaminika unayehusudia. Kuwa na mtandao wa karibu wa wanawake unaoweza kuzungumza nao, ni njia nzuri ya kuhisi umeungwa mkono.
2. Ni sawa kujiandaa mbele.
Ikiwa dhana ya kupata hedhi yako bila kutarajia inakufanya uwe na wasiwasi, basi mbona usiweke bidhaa kadhaa kwenye mfuko wako. Kuweka pedi za hedhi, vitambaa, na chupi kipuri ya kubadilisha kwa mapenzi yako mwenyewe kunaonyesha kuwa umejiandaa daima. Ni kawaida hedhi yako kutofanana kidogo kwa mara ya kwanza, hivyo unaweza anza kuvaa pedi siku chache kabla ya kuanza. Pia ni wazo nzuri kumaki tarehe zako za hedhi kwenye kalenda ili uweze kupata ufahamu wa mzunguko wako wa hedhi.
3. Hedhi sio za aibu.
Nilipokuwa msichana mdogo, nilianza hedhi yangu bila kutarajia katika duka la vyakula. Nilikuwa nikinunua matunda kadhaa, wakati mwanamke mzee aliponiguza begani kuniambia kuwa nilikuwa nikivuja kupitia kaptura yangu. Hata hivyo, hakunicheka, au kunifanya nijihisi kama kulikuwa na jambo baya nami. Alinishika mkono wangu polepole na kunionyesha msalani. Ingawa nilihisi aibu kidogo, fadhili zake zilifanya nigundue kwamba hakuna kitu cha kuwa na aibu. Wakati mwingine tunapata uvujaji au wakati mgumu, lakini hili sio jambo la kujisikia vibaya.
Kwa hivyo kumbuka – hedhi ni hatua nyingine katika safari yako ya kuwa mwanamke mzuri uliyezaliwa kuwa! Hazibadili ulivyo kama mtu na kwa hakika hazikufanyi mchafu. Ni sehemu tu ya asili na ya afya ya maisha yetu. Sasa ikiwa watu wanajaribu kukutendea tofauti unapokuwa na hedhi yako, unaweza kujisimamia na kuelezea UKWELI huu!
Share your feedback