Ninataka kuwa kama wao!
Kila mwaka tarehe 8 Machi dunia husherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Napenda Siku ya Wanawake maana ni fursa ya kusherehekea wanawake duniani kote. Hawa ndio wanawake 3 wanaonihamasisha sana maishani mwangu
Wa 1 ni bibi yangu ! Ninampenda sana bibi yangu. Yeye ni malkia machoni pangu. Alianzisha uriithi wa wanawake wenye nguvu katika familia yangu. Alipokuwa na umri wa miaka 23 aliondoka nyumbani na kuhamia nchi mpya kabisa ili kuanzisha maisha yake mwenyewe.
Ingawaje aliishi katika nchi ya kigeni, bila kumjua yeyote, hakuruhusu hilo liwe pingamizi dhidi ya ndoto zake. Alifanya uamuzi wa kuwa na nguvu na ujasiri kila siku. Ananihamasisha kuwa mstadi na kufuata udadisi wangu.
Wa 2 ni mama yangu ! Bibi yangu lazima alimfundisha mama yangu kila kitu kwa sababu pia yeye ni wa kushangaza. Mama yangu ni mwema, mwenye upendo na ufahamu. Yuko nami wakati wote ninapomhitaji. Nakumbuka nilipoanza kufuata ashiki yangu ya kuigiza. Yeye aliniunga mkono wakati wote. Nilipohisi kama sitoshi, alinitia moyo na akahakikisha kuwa sikati tamaa.
Mama yangu alinifundisha kuhusu uvumilivu. Safari ya kutimiza ndoto zako si rahisi ila unafaa uendelee kupiga hatua za mtoto na kusonga mbele.
Wa 3 ni dada yangu mkubwa ! Ingawa yeye ni mkubwa kwangu kwa miaka 5, bado ni rafiki yangu wa dhati. Tulipokua, tulifanya kila kitu pamoja. Yeye hakuniacha kamwe. Anafanya bidii sana shuleni na daima hupata alama nzuri. Baada ya kutoka shule, yeye hujitolea kwa hisani kuwafundisha wasichana wengine ambao hawako shule. Huu ni wema kiasi gani?
Dada yangu mkubwa amenifundisha umuhimu wa kuwasaidia wasichana wengine. Mara zote husema, "Kama wewe peke yako waweza kutimiza ndoto yako basi si kubwa ya kutosha." Katika safari ya kutimiza ndoto zako ni muhimu kuandamana na watu. Msichana mmoja anaposhinda, wasichana duniani kote wanashinda!
Share your feedback