Nani ana haki zaidi?
Siku ya kwanza kurejea shuleni, Tammy alishikwa makalio na mvulana aliyekuwa darasa la mbele. Haikuwa siku ya kwanza hilo kutendeka. Lakini ulikuwa wakati wa kusema ‘haitakubalika tena!’ kwa wavulana shuleni kutomheshimu yeye au msichana yeyote yule. Kwa hivyo wakati huu Tammy aliamua kupambana na wanyanyasaji wake – na akashinda!
Hivi ndivyo alifanya:
Jua haki zako: Tammy alijua tabia hii haikubaliki. Alijua kwamba wasichana walikuwa na haki ya kutoshikwa na haki ya miili yao na uhuru wao kuheshimiwa. Wasichana wana haki sawa za kufurahia masomo yao kama wavulana. Hangekubali tena majibu ya walimu wake kwamba ‘wavulana ni wale wale’.
Amsha jamii: Tammy alikusanya hadithi za wasichana wa darasa lake na wa shule yake waliopitia haya. Alishtuka jinsi wasichana wengi walivyokuwa na matokeo kama yake na walikuwa wamekasirika pia kwamba wavulana hawakuwa wakiadhibiwa. Alishiriki hadithi hizi na wazazi wake, walioshiriki na wazazi wengine hadi suala hili likawasilishwa shuleni.
Usiwasikilize maadui: Watu watakuambia usizungumze. Lakini kama jambo halikufurahishi au linadunisha haki zako, kuzungumza ndio jambo bora zaidi unaweza fanya. Kama Tammy, unaweza kuzungumza na watu unaowaamini. Dada yako mkubwa, wazazi wako, mwalimu au marafiki zako – anayekubaliana nawe. Sikiliza watu wanaokupenda na uwapuuze maadui.
Miliki uwezo wako: Fahamu kwamba una uwezo wa kubadilisha mambo. Usikubali watu wakufanye uamini kwamba kuwa msichana ni dunikuliko kuwa mvulana. Kila siku, duniani kote, wasichana wachanga na wanawake wanajenga tena jamii zao. Hata matendo madogo ya ujasiri, kama kuuliza mtu kama ako sawa, yanaweza kuwa na athari kubwa.
Kwa kuzungumza na kushiriki sauti za wasichana wengine, Tammy aliweza kusukuma shule ambayo ilikubali kuweka adhabu kali kwa wavulana wanaonyanyasa wasichana shuleni. Wakati mwingine mtu akijaribu kukuambia ‘wavulana ni wale wale’, jua una haki ya kupaza sauti na kukataa. Sio lazima upambane nao kama Tammy, lakini unaweza kuwa macho kuwalinda wasichana wengine wanaopitia hali sawa na yako. Umoja ni nguvu na kwa pamoja sauti zenu zinaweza kuwa mgurumo.
Share your feedback