Nilituma Picha kwa mvulana

Laiti singetuma

Mimi na Peter tumekuwa marafiki kwa muda mrefu. Kila usiku tunazungumza kwenye simu, wakati mwingine kwa masaa kadhaa. Wiki chache zilizopita, aliniuliza nimtumie picha ya uchi wangu. Nilicheka kwanza na nikamwambia “Haiwezekani!” Alituma jumbe nyingi akiomba picha moja. Nilipuuza nikitumai angechoka kuomba.

Baadaye, siku moja tulipokuwa tunaenda nyumbani kutoka shule, aliniambia tushindane mbio. Akasema nikishindwa, nitahitajika kutuma picha ya uchi wangu. Sijashindwa bado kwa hivyo nilikubali. Lakini, kwa namna fulani – nilishindwa.

Nilimtumia picha ya bra yangu ili anyamaze. Baadaye akaniomba moja bila bra – akisema nilimuahidi. Nilikubali na nikamtumia picha bila nguo kifuani.

Nilijuta mara moja. Nilimuomba aifute lakini akakataa. Nilichanganyikiwa, nilidhani alikuwa rafiki yangu.

Mama yangu aligundua nimeanza kunyamaza na kuhuzunika. Niliogopa kuzungumza naye kuhusu hili kwani sikutaka akasirike.

Nilijua kutokana na maongezi tuliyokuwa nayo kwamba alitaka nimwendee ikiwa niko hatarini au nilikuwa nimeumizwa na mtu. Kwa hivyo nikaamua kwamba ningemuamini na hata kama angekasirika kiasi, alikuwa mtu ambaye angenisaidia.

Nilimuuliza kama ningeweza kuzungumza naye kuhusu jambo la siri. Pia nilimuuliza kama angeweza kuwa na huruma kwangu, kwani nilijua nilikuwa nimekosea. Alikubali. Nilipomuambia kilichotendeka alishtuka na alivunjika moyo, lakini kama alivyoahidi alibaki kuwa mtulivu na tukafanikiwa kuwa na mazungumzo mazuri.

Aliniambia, wasichana wanapobaleghe, wanapata uangalifu usiofaa kutoka kwa wavulana. Hata tunaodhania ni marafiki zetu wanaweza kutushinikiza kufanya mambo ya ngono tusiyofurahia. Aliniambia kuwa kuzungumza na watu ninaowaamini wanaoweza kunisaidia na kunipa ushauri ndio jambo bora sana kufanya ninapohisi ninashinikizwa kufanya jambo. Kwa pamoja, tulizungumzia mawazo ya jinsi ya kukabiliana na hali ile. Alinisaidia sana.

Tuliamua kuzungumza na Peter kwa pamoja na alinifunza jinsi ya kuzungumza kuhusu hisia zangu za kuchanganyikiwa na kukasirika kwa Peter. Hii ilisaidia sana Peter kujua kwamba matendo yake yaliniumiza na aliifuta ile picha kwa hiari. Natamani ningezungumza na mama yangu mapema – hakuna tatizo asiloweza kusuluhisha!

Iwe ni mama yako, dada yako, rafiki yako au jirani yako – pata mtu utakayeweza kumwendea wakati shinikizo imekuwa nyingi.

Share your feedback