Jiamini. Usiwe na hofu.
Kwa kawaida hedhi huhusishwa na maumivu, chunusi, kubadilika kwa hisia na kuaibika kwa hisia LAKINI, niko hapa kukuambia kuwa haifai kuwa hivyo.
Unapokuwa na hedhi, watu wanaweza kukuambia kila aina ya mambo kama vile "baki kitandani siku yote", "usicheze mchezo", au "usimwarifu mtu yeyote kwamba una hedhi", lakini hufai kuwasikiliza. Ikiwa unahisi kufanya kitu, kifanye. Usimruhusu yeyote kuwa kizuizi, dada! Shukrani kwa Springster, sasa huu ndiyo mtazamo wangu kwa kila kitu katika maisha.
Mwezi uliopita nilikuwa na mchuano mkubwa. Kila siku mimi na timu yangu tulifanya mazoezi. Tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda michuano ya taifa katika mbio za kupokezana. Kila kitu kilikuwa shwari tukikaribia mchuano. Lakini siku moja kabla, katikati ya mazoezi hedhi zangu zikatokea bila kutarajia!
Uzuri sikupata madoadoa yoyote, lakini nilihitaji kuondoka mazoezini mapema ili kupumzika kabla ya siku iliyofuata. Ni mamangu pekee aliyejua kuhusu hedhi zangu na niliona aibu kumwarifu kocha wangu wa kiume kwamba nilikuwa na hedhi. Mimi pamoja na wasichana tulijaribu kuwaza visingizio vya ghafla vile tungeweza kumwambia bila kusema ukweli. Tulicheka sana tulipokuwa tunapanga visingizio vya ujinga wakati Gloria alipotuarifu kuwa Kocha alikuwa na binti mkubwa. Kuna uwezekano alikuwa ameanza kupata hedhi, kwa hivyo hapakuwa na chochote cha kuonea aibu. Gloria alisema ukweli. Ingawa wanaume hawapati hedhi lakini wana mama, dada na wake ambao hupata, hivyo wanaelewa.
Hata hivyo, huku nikiwa na uoga na aibu kidogo, nilikwenda kwa Kocha na nikamwarifu kuwa nilikuwa na hedhi. Yale aliyosema ni hakuna tatizo, angempigia mamangu ili aweze kuja kunichukua. Loo. Mazungumzo yalikuwa rahisi sana!
Siku iliyofuata niliamka nikihisi kama bingwa. Na kwa mtazamo huo nilijikaza na tukaweza kushinda mbio hizo! Nilipovuka mstari wa kumalizia mwanahabari alikuja ili kuwa na mahojiano na mimi.
“Hongera Kwassi! Unajihisi vipi?” akauliza.
Nikajibu, “Najihisi vizuri! Jana nilipatwa na hofu kidogo wakati hedhi zangu zilipotokea, lakini niliamua kuwa sitokubali ziwe kizuizi. Nilijishughulisha tu na mbio na nafurahi sana kwa matokeo. “
Baada ya kuamua kumweleza Kocha kuhusu hedhi zangu, sikuona haja ya kuaibika na chochote. Watu wengine hawaamini kwamba nilizungumza kuhusu hedhi zangu kwenye TV ya kitaifa lakini nani anajali! Hedhi ni za kawaida na hakuna chochote cha kuonea aibu kuhusiana nazo. Nafurahi tu timu yangu ilishinda!
Share your feedback